Timu ya soka ya Simba leo itajitupa uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kuwavaa washiriki wenzao wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika timu ya kandanda ya AS Vita kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo unaotazamiwa kuwa wa kufa na kupona ili timu ya Simba iweze kupata nafasi ya kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, hivyo inaifanya Simba kuhakikisha inashinda mchezo huo kwanza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele pili kufuta uteja kwa timu hiyo ambapo kwenye mchezo wa awali uliopigwa mjini Kinshansa AS Vita iliichapa Simba 5-0.
Mchezo huu wa leo utarushwa na vituo mbalimbali vya redio na runinga.
Dua zetu kwa Simba na watanzania wote tuungane kuiombea.


No comments:
Post a Comment