Latest News

Habari Kuu

Mwanza

Magazeti

Movies255

Recent Posts

Monday, July 22, 2019

SHAKA CCM IPO IMARA ITAHIMILI MISUKOSUKO

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka amesema licha ya Chama chao kupitia katika nyakati ngumu kipindi hiki lakini bado kipo imara.

Pia amesema Rais John Magufuli yupo imara kuendesha Chama hicho na anahimili na kupambana na mawimbi yanayoambatana na pepo za kusi na kaskazini.

 Akizungumza juzi mkoani humo wakati wa Mkutano wake na wananchi na maofisa mbalimbali Shaka alisema jahazi la CCM halijawahi halijawa kukabidhiwa mtu dhaifu wala legelege,hivyo litavuka salama na kuendelea kuwa na umoja na Mshikamano.

Alisema kitendo cha kumbugudhi Mwenyekiti wa Chama hicho katika kipindi chake cha uongozi wa miaka 10 ambacho hakijamalizika,hakiwezi kuvumiliwa.

Alisema mtu yeyote Anayeweza kutenda jambo hilo atahesabiwa kama baharia mdandia meli asiye na cheti cha kazi hiyo au hati ya kusafiria hivyo si ajabu atatoswa mkondoni.

"nawahakikishia tutavuka salama na tutaendelea kuwa wamoja wenye upendo na mshikamano chini ya Mwenyekiti na Rais Magufuli CCM imepitia katika nyakati ngumu sana na imeendelea kuwa imara siku hadi siku nahodaha wetu ndani ya chombo usukani ameushikilia vyema anahimili na kupambana na mawimbi makubwa yanayoambatana na pepo za kusi na kasikazi mabaharia wote wako makini na abiria wametulia alisema na kuongezea kuwa;


"Chama ndicho kinachompa amana na dhamana mwanachama wake kwa miaka 10 haiwezekani tena chama hicho hicho kimwambie hebu kaa pembeni mpishe huyu wakati hajamaliza muda wake ,dharura hiyo haipo haipo na haijatokea kwenye historia ya CCM tangu mwaka 1977,"alisemA sHAKA .


"Viongozi wa CCM ngazi zote hakikisheni mnachapa kazi ,timizeni wajibu wenu wa kikatiba na kanuni ,kwani CCM ni chama kikubwa na imara mno,kina viongozi wazoefu ,walio na busara na hekima"alisema na kuongeza "wapinzania wanaomba CCM igawanyike wanaomba CCM igawanyike halitatokea ,CCM ina mbavu za kuhimili aina ya misukosuko na dhoruba hatimaye kitavuka kikiwa salama," alisema Shaka 


Aliwataka Watanzania waendelee kusimama pamoja na Rais Magufuli wakati wote kwa kuwa ni kiongozi aliyeamua kwa dhati kuwatumikia wananchi akijali dhiki na shida na kutaka kuwafikisha kwenye nchi ya neema naustawi.


Mwisho:Chanzo Majira

Saturday, March 16, 2019

Simba kuingia robo fainali KBA (Klabu Bingwa Afrika)?


Timu ya soka ya Simba leo itajitupa uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam kuwavaa washiriki wenzao wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika timu ya kandanda ya AS Vita kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo unaotazamiwa kuwa wa kufa na kupona ili timu ya Simba iweze kupata nafasi ya kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, hivyo inaifanya Simba kuhakikisha inashinda mchezo huo kwanza kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele pili kufuta uteja kwa timu hiyo ambapo kwenye mchezo wa awali uliopigwa mjini Kinshansa AS Vita iliichapa Simba 5-0.
Mchezo huu wa leo utarushwa na vituo mbalimbali vya redio na runinga.
Dua zetu kwa Simba na watanzania wote tuungane kuiombea.


Tuesday, March 12, 2019

KATIBU MPYA WA CCM MKOA WA MWANZA ASAINI KITABU KWAMKUU WA MKOA WA MWANZA

Mapema jana tarehe 11/3/2019 mara tu baada kukabidhiwa ofisi ya ccm mkoa wa mwanza alitembelea ofisi ya mkuu wa mkoa wa mwanza na kusain kitabu cha wageni

Monday, February 18, 2019

TUNAWAKARIBISHA WADAU WOTE NA WAPENDA HABARI KUTANGAZA BIASHARA  ZENU NA BLOGG YETU YA KIM TZ

Thursday, April 28, 2016

VIONGOZI WA KISIASA WAFANYA BIASHARA,WATAKIWA KUWAJALI NA KUWATHAMINI WATOTO WENYE ULEMAVU


Na FAHADI SIRAJIViongozi wa kisiasa, wafanyabiashara, viongozi wa kiserikali na wafanyajazi
wametakiwa kuwajali na kuwathamini sana watoto  wenye ulemavu na wanaoishi
kwenye mazingira magumu kwani wao pia  ni binadamu wanao sitahili kupata
haki na mahitajj muhimu ya kibinadsmu
Hayo yamebainishwa na leo na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu
Shaka wakati alipotembelea shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo
mkoani Kilimanjaro yenye jua huduma watoto wenye ulemavu wa viungo na MTI
ndio wa akili.
Alisema kuwa ni muhimu kuwajali sana watoto wenye ulemavu kwani
wakitengenezwa vizuri na kuandaliwa vizuri kwa kupewa elimu  watakuwa
viongozi wazuri wa baadae.
Aidha alivitaka vyama Vya siasa vijielekeze kutatua changamoto na ma tatizo
ya watoto ambao ni Walemavu na sio kuendeleza Kufanya siasa ata sehemu
ambayo aitakiwi siasa.
"napenda kuviambia vyama vingine vya siasa sasa ivi uchaguzi imeisha ni
kipindi cha kufanya kazi na kuachana na siasa sasa ivi ni kipindi cha
kufanya kazi na kutatua ma tatizo ya wananchi " alisema Shaka.
Kwa upande wa Mkuu wa shule ya msingi Mreyai, Nuruel Laizer alisema kuwa
shule hiyo inahudumia wanafunzi wenye Mtindio wa akili na wanafunzi ambao
ni walemavu wa viungo ambapo alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa chakula cha wanafunzi, ukosefu
wa vitanda na mgodoro ya kulalia Wanafunzi ambao ni walemavu ,baskeli kwa
ajili ya watoto ambao ni walemavu wa miguu.
Alisema kuwa Wanafunzi hao wanakaa katika ma bweni apo shule ni lakini
wanaupungufu mkubwa wa vitanda na mgodoro  kwani vitanda ambavyo wana vitu
mia wameviazima kutoka kwa watu na mda wowote wenyewe wanaweza kuja
kuchukuwa.
Aliomba serekali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia kitu icho
ili watoto hao waweze kuishi kwa amani na furaha kama watoto.
"watoto hawa wanawazazi lakini wazazi hao hawana uwezo na ndio maana wa me
wamewaleta Hapa ili wapate elimu hivyo tu naomba sana serekali na wadau
mbalimbali wajitokeze kutusaidia"alisema laizer
Shule hii ya msingi Mreyai imepata msaada wa chakula, maharage, malindi,
sabuni, mafuta, miswaki na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu
Shaka aliaidi kusaidia shule hii vitanda Nane na mgodoro kwa ajili ya
wanafunzi hawa wenye ulemavu wa viungo pamoja na Mtindio wa ubongo.

 Wanafunzi wa shule ya msingi Mreyai iliyopo wilayani Rombo mkoa wa kirimanjaro wakisikiliza kwa makini ugeni wa kaimu katibu mkuu uvccm taifa Shaka Hamdu Shaka
 Wanafunzi na ugeni ukisikiliza Risala iliyo somwa na mmoja wa wanafunzi walemafu katika shule hiyo
 Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akipokea Risala ya Wanafunzi
 mkuu wa shule ya msingi Mreyai Nuruel Laizer  wa kwanza kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Rahibu Juma akifuatiwa na kaimu  katibu mkuu UVCCM taifa katika makabidhiano ya baadhi  ya msaada ambao ulipelekwa shuleni hapo
 mkuu wa shule ya msingi Mreyai Nuruel Laizer  wa kwanza kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa kilimanjaro Juma Rahibu Juma akifuatiwa na kaimu  katibu mkuu UVCCM taifa katika makabidhiano ya baadhi  ya msaada ambao ulipelekwa shuleni hapo
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mreyai
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mreyai
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka akizungumza na moja ya Wanafunzi wenye ulemavu
 Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka akipanda mti
 Wanafunzi wa Shule ya msingi Mreyai wakifurahi pamoja na
-Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka H Shaka

Tuesday, April 26, 2016

MWENYEKITI WA CCM MOSHI VIJIJINI AUAWA KIKATILI


Na Mwandiahi Wetu.Kilimanjaro

  Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi Kata ya Okaoni wilaya ya Moshi Vijijini mkoani kilimanjaro Sebastian Joseph Kimati amevamiwa na majambazi nyumbani kwake usiku wa kuamkia juzi na kumkatakata mapanga hadi kumuua.
Habari toka kwa mashuda wa tukio hilo  pia  kuthibitishwa na ofisi ya mkuu wa kituo kidogo cha polisi kata ya Okaoni zimesema kundi linalodhamiwa kuwa na watu zaidi ya saba walivamia nyumbani kwa marehemu Kimati na kumpotezea maisha .
Mtu mmoja wa karibu katika familia ya marehemu aitwaye Julius Mmari alisema majambazi hao walifika nyumbani kwa ndugu yake takriban majira ya saa 6 usiku, wakaanza kupiga matofali dirishani na kusukuma mlango wa mbele ndipo marehemu Sebastian alipochungulia kupitia dirishani kwake  na kuwatambua huku akiwaita kwa majina baadhi ya majambazi hao.
Alisema baada ya marehemu kuwaita kwa majina majambazi wengine walifanikiwa kuvunja mlango wa mbele na walipokutana ukumbini ana kwa ana ndipo walipomshambulia kwa kutumia mapanga ya uso na sehemu kubwa ya kichwa.
Aidha watu hao makatili pia walimshambulia mke  wa marehemu kwa kumpiga mapanga pamoja na mama  wa marehemu Sebastian.
"Yasemekana walikuwa wakimtaka sebasti  afungue mlango na atoe fedha kwasababu aliuza kiwanja chake, walipoanza kumpiga akawapa kiasi cha fedha huku  majambazi hao  wakimlazimisha afunge mlango wa duka lake ambako wakiamini pia wangepata fedha "anaeleza julius .
Juhudi za kumpata kamanda wa Polisi Mkoa wa kilimanjaro hazikufanikiwa.
 
PICHANI: Katibu wa  siasa na Uenezi ccm wikaya ya Moshi vujini Hussein Jamal akimfariji na kumpa mkomo wa pole kaka wa aliyekuwa Mwenyekiti wa ccm kata Okaoni marehemu Sebastian Joseph Kimati.
 Katibu wa  siasa na Uenezi ccm wikaya ya Moshi vujini Hussein Jamal akizungumza na Familia ya Marehemu Sebastian Joseph Kimati.
Eneo la Nyumba ya Marehemu Sebastian Joseph Kimati

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM SHAKA HAMDU SHAKA AKAMILISHA ZIARA YAKE YA KUIMARISHA CHAMA NA JUMUIYA ZAKE MOSHI MJINI MKOANI KILIMANJARO

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA (MNEC), SHAKA HAMDU SHAKA (KULIA),  AKISALIMIANA KATIBU WA CCM MKOA WA KILIMANJARO (KUSHOTO) BAADA YA KUWASILI KATIKA OFISI ZA UVCCM MKOA WA KILIMANJARO.
 KAIMU KATIBU MKUU UVCCM (MNEC) SHAKA HAMDU SHAKA AKISAINI DAFTARI LA WAGENI.
 KATIBU WA UVCCM MKOA WA KILIMANJARO, YASSIN LEMA AKIMFAFANULIA JAMBO KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA (MNEC) SHAKA HAMDU SHAKA 

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM (MNEC)SHAKA HAMDU SHAKA AKISALIMIANA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA CHAMA NA JUMUIYA MARA BAADA YA KUWASILI KATIKA OFISI YA CCM WILAYA YA MOSHI MJINI
 AKISAINI KITABU CHA WAGENI NA KUPOKEA TAARIFA FUPI YA UVCCM WILAYA YA MOSHI MJINI.

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA (MNEC)SHAKA HAMDU SHAKA AKIPANDA MTI WA KUMBUKUMBU NJE YA OFISI YA CCM WILAYANI MOSHI MJINI.

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA (MNEC) SHAKA HAMDU SHAKA AKIKABIDHI ZAWADI KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA.
 KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA (MNEC) SHAKA HAMDU SHAKA AKIKABIDHI ZAWADI KWA KITUO CHA WATOTO YATIMA.
 AKIOSHA GARI MARA BAADA YA KUZINDUA SHINA LA WAKEREKETWA LA CAR WASH  TAWI LA MAKANGE LILILOPO KATA YA MAJENGO MAPYA
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Juma Raibu  ambaye ameshinda kesi ya Udiwani katika Kata ya Mbomambuzi, akisalimia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bomambuzi, Pasua sokoni Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati wa mkutnao wa hadhara .
 Wananchi wakimshangilia KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA (MNEC)SHAKA HAMDU SHAKA
 AIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA (MNEC)SHAKA HAMDU SHAKA AKIKABIDHI  KADI 200 KWA WANACHAMA WA UVCCM NA CHIPKIZI KATIKA MKUTANO WA HADHARA 

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA KAMDU SHAKA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO WA HADHARA MAENEO YA PASUA KICHWA AMBAPO ALISEMA ''NIWAPONGEZENI SANA KWA KUKIAMINI CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA UCHAGUZI MKUU NA NIWAHAKIKISHIE HAKUNA CHAMA IMARA TANZANIA ZAID YA CCM, KUPITIA RAIS JOHN JOSEPH POMBE MAGUFURI MPAKA KUFIKIA 2020 TUTAKUA TUMEONDOA NA KUTIMIZA AHADI ZETU  TULO WAAHIDI NDANI YA ILANI YA CCM''.
KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA (MNEC)SHAKA HAMDU SHAKA AKIHUTUBIA UMATI WA WANANCHI WA KATA YA BOMA LA MBUZI KATIKA VIWANJA VYA PASUA SOKONI.
  (PICHA NA FAHADI SIRAJI)