Latest News

Tuesday, April 26, 2016

MWENYEKITI WA CCM MOSHI VIJIJINI AUAWA KIKATILI


Na Mwandiahi Wetu.Kilimanjaro

  Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi Kata ya Okaoni wilaya ya Moshi Vijijini mkoani kilimanjaro Sebastian Joseph Kimati amevamiwa na majambazi nyumbani kwake usiku wa kuamkia juzi na kumkatakata mapanga hadi kumuua.
Habari toka kwa mashuda wa tukio hilo  pia  kuthibitishwa na ofisi ya mkuu wa kituo kidogo cha polisi kata ya Okaoni zimesema kundi linalodhamiwa kuwa na watu zaidi ya saba walivamia nyumbani kwa marehemu Kimati na kumpotezea maisha .
Mtu mmoja wa karibu katika familia ya marehemu aitwaye Julius Mmari alisema majambazi hao walifika nyumbani kwa ndugu yake takriban majira ya saa 6 usiku, wakaanza kupiga matofali dirishani na kusukuma mlango wa mbele ndipo marehemu Sebastian alipochungulia kupitia dirishani kwake  na kuwatambua huku akiwaita kwa majina baadhi ya majambazi hao.
Alisema baada ya marehemu kuwaita kwa majina majambazi wengine walifanikiwa kuvunja mlango wa mbele na walipokutana ukumbini ana kwa ana ndipo walipomshambulia kwa kutumia mapanga ya uso na sehemu kubwa ya kichwa.
Aidha watu hao makatili pia walimshambulia mke  wa marehemu kwa kumpiga mapanga pamoja na mama  wa marehemu Sebastian.
"Yasemekana walikuwa wakimtaka sebasti  afungue mlango na atoe fedha kwasababu aliuza kiwanja chake, walipoanza kumpiga akawapa kiasi cha fedha huku  majambazi hao  wakimlazimisha afunge mlango wa duka lake ambako wakiamini pia wangepata fedha "anaeleza julius .
Juhudi za kumpata kamanda wa Polisi Mkoa wa kilimanjaro hazikufanikiwa.
 
PICHANI: Katibu wa  siasa na Uenezi ccm wikaya ya Moshi vujini Hussein Jamal akimfariji na kumpa mkomo wa pole kaka wa aliyekuwa Mwenyekiti wa ccm kata Okaoni marehemu Sebastian Joseph Kimati.
 Katibu wa  siasa na Uenezi ccm wikaya ya Moshi vujini Hussein Jamal akizungumza na Familia ya Marehemu Sebastian Joseph Kimati.
Eneo la Nyumba ya Marehemu Sebastian Joseph Kimati

No comments:

Post a Comment