Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, bwana Gerson Msigwa inasema kuwa sherehe hizo ambazo zingegharimu zaidi.ya shilingi bilioni 2 za kitanzania zimefutwa mwaka huu na badala yake pesa hizo zimeelekezwa kwenye upanuzi wa barabara ya Mwanza -Airport.
Endapo kama sherehe ya mwaka huu ya Muungano ingefanyika fedha zilizotengwa zingetumika kugharamia shughuli za maadhimisho hayo kama vike; vinywaji, chakula, gwaride la jeshi n.k.
Hii inakuwa ni mara ya tatu kwa Rais Magufuli kufuta sherehe za kitaifa na kuagiza fedha zielekezwe kwenye shughuli za maendeleo baada ya hapo awali kufuta maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) tarehe 9/Desemba/2015 na kabla ya hapo alifuta maadhimisho ya siku ya UKIMWI kitaifa kisha kuagiza fedha zielekezwe kununulia dawa za kupunguza makali ya virusi kwa waathirika (ARVs).
Isome hapa kwa ukamirifu taarifa hiyo

No comments:
Post a Comment