Latest News

Sunday, April 3, 2016

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa atikisa Mwanza, apokea wanachama wapya 700

Na, Hussein Egobano - KIMTZ Entertainment.

Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa ndugu Shaka H. SHAKA leo ameendelea na ziara yake hapa mkoani Mwanza na kuhutubia Umoja Wa Vijana Wa CCM wilaya ya Ilemela katika mkutano uliofanyika kuanzia saa tisa Alasiri hadi majira ya saa kumi na mbili jioni kwenye uwanja wa Magomeni, Kirumba.

Katika mkutano huo wa Kihistoria Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa alipokea wanachama wapya wa UVCCM mia saba.
Mkutano.huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama akiwemo Katibu Mkuu wa chama mkoa ndugu Miraji Mtaturu.

No comments:

Post a Comment